Kitaifa

TUNDU LISSU NA FALSAFA YA PUNDA

Juzi Tundu Lissu katamka kwenye moja ya mahojiano mtandaoni kwamba Mheshimiwa Rais Samia kaingilia Bunge na hastahili staha katika kumkosoa. Kauli ya Tundu Lissu imenikumbusha stori ya Punda. Kwamba ukikuta ana shida ukamnyanyua na kumuweka sawa, shukrani yake ni mateke.

Lissu alipigwa risasi zaidi ya 20, kati ya viongozi watatu wakuu wa Serikali ni Samia pekee aliyekwenda kumjulia hali akiwa hospitalini Nairobi. Lakini pia ni Samia huyu huyu aliyemuomba Mbunge wa Mpendazoe marehemu Turky kutoa ndege binafsi kumuwahisha Lissu hospitali.

Lissu kaishi uhamishoni kwenye apartment ndogo akijibana na watoto na mkewe nchini Ubelgiji, ni Samia huyu huyu kamuwezesha kurudi nchini kwa sababu ya utu wake wa kuheshimu Katiba. Mbona mtangulizi wake aliisigina Katiba na hakuna aliyesema neno? Nini kimemzuia Samia kufanya hivyo? UTU wake kama binadamu mwenye hofu ya Mungu na muungwana.

Lissu alifika mahali hana pasipoti ya nchi yoyote, ni Samia aliyehakikisha anapata pasi yake ili aweze kusafiri kwa uhuru.

Lissu huyu alinyimwa stahiki zake zote na Bunge ikiwemo fedha ya matibabu na kiinua mgongo, akawa anaishi kwa hisani ya wazungu wa Umoja wa Ulaya. Ni Samia aliyehakikisha Lissua anapata si tu stahiki zake zote lakini hata kiinua mgongo chake Bungeni.

Wakati Samia anafanya yote hayo, Lissu hakuona Samia anaingilia Bunge kulazimisha wamlipe, hakuona Samia ni wa hovyo, hakuona Samia hafai. Kwa nini? Kwa sababu ilikuwa ni maslahi yake binafsi. Ilikuwa mrija wa chakula kwenye tumboni kwake.

Lissu, unapokosoa kumbuka staha, kumbuka utu wa kiongozi mkuu wa nchi, kumbuka hisani, na kuondoa unafiki.

*Ndimi Sagati Wachiuri*
Butiama, Mara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi