Connect with us

Kitaifa

Tafakari Fupi: Rais Samia ni kiongozi, au ni mwanasiasa?

Mchungaji mashuhuri marehemu Myles Munroe aliwahi kusema hata siku moja usidhani mifumo tuliyo nayo duniani itatuzalishia viongozi, badala yake inatuzalishia wanasiasa. Akaongeza kuwa ni mara chache sana mifumo hii ya kiutawala huzalisha viongozi ila mara nyingi huzalisha tu wanasiasa. Lakini waliokuwa wakimsikiliza walitaka kufahamu kuna tofauti gani kubwa kati ya kiongozi na mwanasiasa. Akawaelezea kuwa tofauti ya kiongozi na mwanasiasa huwa katika namna wanavyowaza na kutenda.

Mwanasiasa huwaza uchaguzi ujao, kwamba ninachofanya leo kitanisaidia nini kushinda uchaguzi uchaguzi ujao? Hivyo mwanasiasa atasema uongo, atapiga ramli, ataua, atafanya kila anachoweza kushinda uchaguzi unaofuta.

Kiongozi kwa upande mwingine yeye hawazi sana uchaguzi ujao bali kizazi kijacho. Ataweza nini afanye ili kizazi kijacho kiwe na maisha bora zaidi. Hataogopa kutishwa na makundi ya wenye fedha wanaohodhi kifisadi mifumo ya nchi yenye kuwanufaisha. Wenye fedha wenye kumiliki biashara na sekta ambazo unyonyaji wake huwanufaisha. Mfano siku za karibuni katika sekta ya bandari Tanzania tumeona tofauti ya kiongozi na mwanasiasa ambayo imetupa sifa ya Rais Samia. Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 25 Tanzania imeshika na mafisadi wanaoneemeka huku wakizidisha gharama za kuingiza bidhaa nchini ambazo hupelekea kuongezaka kwa bei za bidhaa kwa mwananchi wa kawaida.

Akiwaza kama kiongozi badala ya kuwaza kama mwanasiasa, leo Rais Samia anapotaka kubadili mifumo kuwa yenye kumpa nafuu mwananchi wa kawaida, mafisadi wanalipa watu kumpinga kwamba kauza, lakini ukweli ni kwamba wanaolipa watu kupinga jambo hili wanaona maslahi yao ya kifisadi yanakwenda kukoma. Ushauri wangu watunze fedha walizo nazo kwa matumizi mengine kwani wanapoteza muda, hawatashinda, hawatashinda, hawatashinda. Wanasahau Rais Samia si mwanasiasa, hatishiki na uchaguzi sababu anajua yuko ndani ya mioyo ya Watanzania na watavuka naye, yeye anawaza maisha ya kizazi cha Watanzania wa leo na kijacho.

George Batenga

Juni 22, 2023

Safarini Mtwara

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi