Connect with us

Kitaifa

Serikali yaongeza muda wa notisi kwa wapangaji Kariakoo

Dar es Salaam. Serikali imeongeza miezi mitatu ya notisi kwa baadhi ya wafanyabiashara na wakazi waliopanga katika nyumba za shirika la nyumba la Taifa (NHC) eneo la Kariakoo hadi Desemba 31, 2023.

Uamuzi huo umetangazwa jana Jumatatu Juni 19, 2023 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula wakati wa mkutano wa pamoja wa wizara hiyo, NHC na uongozi wa wapangaji kufuatia maombi ya wapangaji hao kuiomba serikali kuwaongezea muda na kuwapa kipaumbele pindi uendelezaji wa maeneo waliyopo utakapo kamilika.

“Kariakoo ni miongoni mwa maeneo yanayotakiwa kufanyiwa maboresho na tunatarijia kuwa baada ya maboresho hayo haitakuwa Kariakoo kama ya sasa, itakuwa nyingine,” amesema Waziri Mabula.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah amewatoa hofu wapangaji kuhusu uendelezaji unatarajiwa kufanyika kwa ubia.

“Nashukuru kwamba wote tunakubaliana na uendelezaji wa eneo la Kariakoo tunatofautiana tu kwenye namna ya uendelezaji,” amesema Abdallah.

Wiki iliyopita ziliibuka taarifa kwamba kuna mbia ambaye ameanza kuwachangisha fedha wapangaji hao kiasi cha Sh2 milioni kila mmoja ili waweze kurejea kwenye nyumba hizo mara baada ya uendelezaji jambo lililokanushwa na NHC.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi