Kitaifa

Ndege ya mizigo na falsafa diplomasia ya uchumi

Dar es Salaam. Serikali iko tayari kushirikiana na sekta nyingine, zinazozalisha mizigo ili kuhakikisha inasafirishwa na kufika kwa haraka katika masoko mbalimbali duniani.

 Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Juni 3, 2023 na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, wakati wa mapokezi ya ndege mpya ya mizigo ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya ‘BOEING 767-300F Air Tanzania Cargo’ iliyowasili nchini.

Profesa Mbarawa amesema ujio wa ndege hiyo utaenda kuwa chachu ya biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine, na hivyo kuendana na utekelezaji wa falsafa ya Diplomasia ya uchumi, ambayo rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiisisitiza sambamba na mahusiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali Duniani.

“Wizara itaendelea kutekeleza jukumu lake kuu na kuandaa sera zitakazosaidia matumizi ya rasilimali kupitia uwekezaji unaofanywa na serikali, ili kuleta matokeo makubwa katika shughuli za ukuaji wa uchumi hapa nchini,” amesema.

“Pamoja na jukumu hilo wizara itaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa sekta za kiuchumi na kijamii pamoja na sekta binafsi, ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa sana,”alisema Profesa Mbarawa.

Aidha Profesa Mbarawa amesema, katika bajeti iliyowasilishwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imeweza kuongezewa ndege, kuboreshewa karakana ya ndege na uendeshaji katika shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi