Connect with us

Kitaifa

Majaliwa: Tanzania haina mgogoro na Denmark

Dodoma. Kufuatiza azima ya Denmark kufunga ubalozi wake nchini, serikali imetangaza kuwa, haina mgogoro na nchi hiyo na kwamba inaendelea na mazungumzo ili kuona Ubalozi wa nchi hiyo unaendelea na shughuli zake nchini.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 11, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye hata hivyo amekiri kuwa nchi hiyo imebadilisha sera zake katika Balozi zote kitu ambacho kimeifanya Tanzania kukosa sifa hizo.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Chakechake Ramadhani Suleiman Ramadhan (CCM) ambaye ametaka kujua kuhusu uvumi kuwa Serikali ya Denmark inaondoa ubalozi wake Tanzania kutokana na nchi hizo mbili kutokuwa na mahusiano mazuri.

Waziri Mkuu amesema hakuna mahusiano mabaya baina ya nchi hizi mbili na kwamba wamekuwa na mazungumzo mazuri kila wakati na mara ya mwisho ni wiki mbili zilizopita ambapo walizungumza na Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

“Tanzania inayo mahusiano na nchi mbalimbali za kibalozi na tumeendelea kuwa na mahusiano mazuri sana na Denmark ikiwemo mahusiano ya kidiplomasia, kisiasa na kiuchumi,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesema kuwa hadi sasa Watanzania wachache walioko Denmark wanaendelea na biashara zao kama kawaida bila ya hofu.

Kuhusu mabadiriko ya Sera, amesema kuwa Denmark kwa sasa wanaweka Ubalozi kwenye nchi ambazo hazina usalama lakini Tanzania imekuwa na usalama hivyo wanatarajia kuondoa ubalozi wao 2024 lakini wanaendelea kuwashawishi waendelee kubaki.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi