Connect with us

Kitaifa

Mpina ahoji ‘hasara’ trilioni 2 ujenzi SGR, Serikali yajibu

Dodoma. Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina (CCM) leo tena ameibana Serikali akihoji ni kwa nini Serikali ilitumia njia ya ‘’single source’ kumpata Mkandarasi CCECC wa Mradi wa SGR LOT 6 kati ya Tabora-Kigoma na kusababisha hasara ya Sh2 trilioni.

Hata hivyo Serikali imejibu leo kuwa, hakuna hasara iliyotokea kutokana na ukweli kuwa Serikali ilifuata taratibu zote katika hatua za manunuzi kwenye mradi huo.

Katika swali la nyongeza Mpina amesema Shirika la Reli (TRC) iliacha kuingia mkataba na kampuni ambayo ingejenga kilomita moja kwa Sh9.1 bilioni badala yake wakaingia mkataba wa Sh12.5 bilioni ambao ameomba mkataba huo uvunjwe kwa sababu ni wa kinyonyaji.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kuhoji kuhusu kinachoitwa ufisadi kwenye ujenzi huo ambao mara nyingi kwenye michango yake haachi kugusia eneo hilo analosema limesababisha hasara kubwa kwa nchi.

Hata hivyo, leo Serikali imesema kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma imeainisha njia mbalimbali za manunuzi ya mkandarasi zinazoweza kutumiwa ikiwemo njia ya hiyo iliyoeliyohojiwa na Mbunge huyo kutoka Kisesa.

Naibu Waziri wa Ujenzi Atupele Godfrey Kasekenya ameliambia bunge kuwa, Manunuzi ya Mkandarasi kwa kipande cha Tabora- Kigoma yalifuata Sheria za Manunuzi ya Umma namba 7 ya Mwaka 2011 na kanuni zake Na. 161 (1) (a)-(c) (Single source Procurement for works) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013.

“Naomba kumfahamisha Mbunge na Bunge lako tukufu kuwa, hakuna hasara yoyote iliyosababishwa na ununuzi wa mkandarasi wa ujenzi wa njia ya reli ya Tabora-Kigoma kwani ununuzi wa mkandarasi ulifuata taratibu zote za manunuzi ikiwemo majadiliano kwa lengo la kuhakikisha gharama sahihi za mradi zinapatikana,” amesema Naibu Mwakibete.

Alisema makadirio ya gharama za kihandisi (Engineering Estimates) yalikuwa Dola 3.066 bilioni sawa na Sh7.2 trilioni ikilinganishwa na gharama halisi za bei ya Mkandarasi baada ya majadiliano ambayo ni Dola Sh2.216 bilioni ambayo ni sawa Sh5.2 trilioni.

“Hii ni baada ya majadiliano yaliyopelekea kuokoa Dola 273.9 milioni ambayo ni Sh632.74 bilioni kutoka kwenye zabuni ya awali ya Dola 2. 5 milioni sawa na Sh5.8 trilioni, Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa utaratibu wa manunuzi kwa njia ya ‘single source’ ndio uliotumika kumpata Mkandarasi YAPI MERKEZI,” amesema Naibu Waziri.

Kuhusu kuvunja mkabata amesema Serikali haitavunja Mkataba huo kutokana na ukweli kuwa kampuni hiyo ndiyo inayojengwa kwa gharama nafuu na kuokoa fedha ukilinganisha na makampuni mengine.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi