Connect with us

Kitaifa

Kampuni iliyonyimwa kazi Pakistan kwa ujasusi yapewa kazi Tanzania

Serikali ya Tanzania imekuwa mbioni kutaka kuongeza mkataba wa kufanya kazi na kumpuni ya SICPA, kampuni ambayo kazi yake ni kubandika tempu kwenye bidhaa mbalimbali za viwandani ili kurahisisha makusanyo ya kodi na kudhibiti bidhaa za kughushi. Aidha, kampuni hiyo imekuwa ikilaumiwa kwa rushwa na vitendo vinavyokiuka sheria na maadili ya kibiashara, ikiwa tayari imefunguliwa kesi mbalimbali za rushwa nchini Uswisi na Brazil na kupigwa marufuku nchini Pakistan. SICPA ni kampuni ya kutoka Uswizi, inayojihusisha na usalama wa bidhaa na ufuatiliaji wa mchakato mzima wa uzalishaji wa bidhaa hizo. Kampuni hiyo inafanya kazi katika nchi zaidi ya 200, ikiwemo Tanzania. SICPA imekuwepo tangu mwaka 1927 na ina historia ndefu ya kufanya kazi na serikali na taasisi nyingine kuhakikisha usalama wa bidhaa.

Licha ya historia yake ndefu, kampuni SICPA inakabiliwa na tuhuma kadhaa za rushwa na vitendo visivyofaa. Mwaka 2018, kampuni hiyo ilishtakiwa na serikali ya Brazil kwa madai ya kuwahonga maafisa ili kushinda mkataba wa tenda. Mwaka 2019, SICPA ilishtakiwa nchini Uswisi kwa madai ya kutoa rushwa ili kupata mikataba za zabuni katika nchi kadhaa za Kiafrika. Aidha, kampuni hiyo imepigwa marufuku kufanya kazi nchini Pakistan baada ya shirika la ujasusi la nchi hiyo, Inter-Services Intelligence, mojawapo ya mashirika bora zaidi ya ujasusi duniani, kuhisi ujasusi wa kampuni hiyo. SICPA, kampuni iliyobadilika kutoka kuuza maziwa na jibini hadi kuuza wino kwa ajili ya kuchapisha fedha za huduma za stempu, kampuni hiyo ni mali kabisa ya familia ya Amon, wafanyabiashara mashuhuri Wakiyahudi wenye uhusiano wa karibu na serikali ya Israel, na shirika la kijasusi la nchi hiyo, MOSSAD.

SICPA pia, inahusishwa na ufisadi katika kujipatia zabuni za serikali nchini Brazil, Ufilipino, Togo, Venezuela, Colombia, na Ghana. Tarehe 27 Aprili 2023, SICPA ilihukumiwa kwa ufisadi na kuamriwa na Mahakama Kuu ya Uswizi kulipa CHF 81 milioni ($90.6 milioni) kutokana na shutuma za rushwa na ufisadi katika nchi mbalimbali inayofanya kazi. Taarifa ya OAG inaonesha kuwa aliyekuwa meneja wa mauzo wa SICPA alitoa rushwa kwa maafisa wa ngazi za juu katika masoko ya Colombia na Venezuela kati ya 2009 na 2011. Mathalan, Katika majira ya joto ya 2021, kampuni hiyo ililipa CHF 135 milioni kwa mamlaka ya Brazil kumaliza migogoro yake ya kisheria na kuendelea kufanya biashara nchini humo.

Licha ya yote, ni jambo la kushangaza kuona kuwa, licha ya mikataba michafu na vitendo visivyo na maadili ambavyo SICPA imehusika kwa makusudi ili kujipatia mikataba ya zabuni mbalimbali duniani, bado kuna nchi kutoka kusini mwa jangwa la sahara, Tanzania, inataka kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo. SICPA ilitunukiwa zabuni ya kusambaza, kusakinisha na kuendesha mfumo wa stempu za kodi za kieletroniki Tanzania mnamo 2017 na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) na mfumo huo ulianza kufanya kazi mnamo 2018. Viwanda vyote vilivyoingizwa chini ya mpango huo (tumbaku, divai, pombe kali, vinywaji laini na maji kati bidhaa nyingi) vililalamika juu ya gharama ya stempu ambazo zilinunuliwa kwa kila bidhaa moja iliyotengenezwa au kuingizwa.

Inakadiriwa kuwa kati ya 2018 na 2021, SICPA ilikusanya karibu TZS 100 kila mwaka, ambazo zinakusanywa na viwanda. Viongozi wa ngazi mbalimbali nchi, kama vile wabunge nchi Tanzania wamekuwa wakiuliza maswali kwanini serikali ya Tanzania bado inatazamia kufanya kazi na SICTA licha ya malalamiko lukuki kutoka kwa wafanyabiashara, na mkataba kati ya Tanzania na SICTA kuonekana dhahiri unainyonya serikali ya Tanzania kwenye mapato.

Kwa mfano, ripoti zinaonyesha kuwa SICPA inakusanya Tsh 8/- kwa kufunga kofia ya chupa moja ya juisi nchini Tanzania wakati serikali inakusanya Tsh 6/-, wakati nchini Kenya kwa bidhaa hiyo hiyo, SICPA inakusanya Tsh 1/- na chini ya Tsh 1/- nchini Uganda mtawalia. Zaidi ya hayo, inaripotiwa kuwa SICPA inatoza zaidi kuliko nchi yoyote katika nchi za Afrika ya Kati Mashariki, ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa viwanda na biashara changa nchini Tanzania.

Serikali ya Tanzania inapaswa kufikiria upya kufanya kazi na SICPA kutokana na historia ya kampuni hiyo ya rushwa na ufisadi. Kuna njia kadhaa ambazo serikali inaweza kuzingatia, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na kampuni nyingine au kutafuta suluhisho la ndani. Hatimaye, uamuzi wa kufanya kazi na kampuni kama SICPA unaweza kuwa na matokeo hasi kwa Tanzania na wananchi wake. Ni jukumu la serikali kufanya uamuzi sahihi kwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji katika shughuli zake zote.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi