Connect with us

Kitaifa

Serikali yaanza marekebisho sifa, vigezo vya ajira

Dodoma. Serikali imeaanza mchakato wa kutafuta namna bora ya kutoa ajira kwa vijana ili kuondoa usumbufu na malalamiko yenye viashiria vya upendeleo, na hivyo kunufaisha vijana wanaojitolea kufanya kazi kada mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete ambaye amesema mchakato wa vikao hivyo atausimamia yeye baada ya kukasimishwa kwake na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora ni George Simbachawene.

Alipokuwa akijibu hoja za wabunge kabla ya kupitishishwa bajeti ya wizara yake, Simbachawene alisema watalifanyia kazi ombi la wabunge kuhusu jinsi gani serikali itatoa ajira kwa vijana na hasa wale wanaojitolea bila kuwa na usumbufu.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Ng’wasi Kamani bungeni, Kikwete amesema mchakato wa kupanga vigezo na sifa za ajira hizo vikao vyake vimeanza Mei 5.

Katika swali la nyongeza Mbunge huyo ametaka kujua ni kwa nini kusiwe na kigezo cha kuwapa upendeleo vijana wanaojitolea badala ya kuwaingiza kwenye kundi la moja kwa moja kwa waombaji.

Katika swali la msingi Mbunge huyo ameuliza iwapo Serikali haioni umuhimu wa kutoa kipaumbele cha ajira kwa vijana wanaojitolea kutumikia Taifa katika kada mbalimbali za utumishi pindi nafasi za ajira zinapotolewa.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo amesema kwa mujibu wa kifungu cha 2.1.2 cha Sera ya menejimenti na ajira kwa utumishi wa umma, ajira kwa nafasi zilizowazi katika utumishi hujazwa kwa ushindani na uwazi kwa kufanya usaili na kupata washindi katika nafasi husika.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi