Kitaifa

Spika Tulia aomba jimbo lake ligawanywe

Telegram

Dodoma. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,” amesema Ummy.

Katika swali la msingi mbunge wa Kilindi Omari Kigua ameuliza ni lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi kutokana na jiografia yake.

Naibu Waziri amesema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi mbalimbali  ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

“Hivyo kwa kuzingatia taratibu na vigezo, muda wa kugawa majimbo utakapofika Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba,”amesema Ummy.

Ummya amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi