Connect with us

Kitaifa

Bunge latangaza nafasi za kazi 42

Dar es Salaam. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza nafasi za kazi 42 katika kada mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake.

Nafasi hizo zinahusisha madereva (6), mchumi (1), mhandisi wa umeme (1), ofisa usimamizi wa fedha (1), mwandishi wa taarifa rasmi za Bunge (10), ofisa Tehama (1), ofisa sheria (1), msaidizi wa maktaba (1) na katibu msaidizi wa Bunge (sheria) nafasi 2.

Nafasi nyingine ni katibu msaidizi wa Bunge (uchumi) – 2, katibu msaidizi wa Bunge (afya ya jamii/menejimenti ya afya ya jamii) – 1, katibu msaidizi wa Bunge (usimamizi wa mazingira) – 1 na katibu msaidizi wa Bunge (sosholojia) – 1.

Vilevile, Bunge limetangaza nafasi ya katibu mahsusi daraja la III (7), mteknolojia wa maabara (1), mfiziolojia (2), msaidizi wa kumbukumbu (1), ofisa kumbukumbu daraja la II (1) na ofisa utafiti (1).

“Sekretarieti ya Bunge, inatangaza nafasi za kazi za Kada mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake. Watanzania wote wenye sifa na uwezo wanaalikwa kutuma maombi yao ili kujaza nafasi za kazi,” inaeleza taarifa hiyo iliyotolewa leo Aprili 21, 2023 na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi.

Mwisho wa kutuma maombi hayo ni Mei 4, 2023 na waombaji wote wameelekezwa kutuma maombi yao Ofisi ya Katibu wa Bunge, Dodoma au kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) ambao http://portal.ajira.go.tz/.

Aprili 12, 2023, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Angela Kairuki alisema Serikali imetangaza ajira 21,200 kwa kada za walimu na afya ambazo maombi yake yalifunguliwa kuanzia Aprili 12, 2023 hadi Aprili 25, 2023.

Kairuki alisema mgawanyo wa nafasi hizo ni kwamba 13,130 zitachukuliwa na walimu wa shule za msingi na sekondari huku afya ikitengewa nafasi 8,070 kwa watumishi wa ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hopsitali.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi