Kitaifa

Dhambi za Kigoda na Kalemani Anatupiwa January Makamba

Wallah hii nchi kichomi Paroko. Uamuzi wa kupeleka chura wa Kihansi Marekani, ulifanywa na Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2000. Waziri akiwa Abdallah Kigoda. Rais alikuwa Benjamin Mkapa.

Mkataba uliisha mwaka 2020. Rais akiwa John Magufuli na Waziri wa Nishati, Medard Kalemani, waliongeza mkataba, vyura wa Kihansi waendelee kuhifadhiwa Marekani.

January aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati Septemba 2021, alikuta mkataba umeshaongezwa. Hajafikisha hata miaka miwili. Takataka zote zielekezwe kwake.

Mnyonge mnyongeni. Haki yake mpeni.

Tangu vyura wa Kihansi wapelekwe Marekani na Kigoda, walifuata mawaziri Edgar Maokola Majogo, Daniel Yona, Ibrahim Msabaha, Nazir Karamagi, William Ngeleja, Sospeter Muhongo, George Simbachawene na Kalemani.

Mnyororo wote wa mawaziri, kila ovu linatupwa kwa January. Ndio kusema, January alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati, aliteuliwa pia kurithi makosa yote ya watangulizi wake, kwa hiyo asemwe, achafuliwe.

Stupid… kwa sauti ya Mama Samia.

Ninyi mnaotaka January ang’oke Wizara ya Nishati. Mnaokesha kutunga ngonjera feki. Kuweni na subira. Ngojeni afanye makosa yake. Sio kumrithisha makosa ya watangulizi wake.

Pumbavu… kwa sauti ya Mama Samia.

Cecilia Mwalumbe,
SAUTI KUTOKA MAJI MATITU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi