Kitaifa
Takukuru yaokoa Sh14.6 bilioni ‘zilizopigwa’ kinyemela
Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 Takukuru imefanikiwa kuokoa Sh14.2 bilioni na Dola 14,571 za Marekani kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi.
Kati ya fedha hizo Sh8.4 bilioni zilitokana na ukwepaji kodi, huku akieleza kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Ameyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Hamduni amesema Sh2.6 bilioni zilidhibitiwa na kurejeshwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyokusudiwa na wananchi waliokuwa wamedhurumiwa katika vyama vya msingi katika mikoa ya Manyara, Rukwa, Katavi, Kigoma, Morogoro, Mtwara, Simiyu, Pwani, Singwe, Tanga na Mwanza.
“Takukuru pia ilifanya uchunguzi na kukamilisha jumla ya majalada 1,188 yakiwemo majalada 16 ya rushwa kubwa. Rushwa kubwa ulihusisha ubadilifu wa fedha za mradi wa mabasi yaendayo haraka ambapo jumla ya Sh8 bilioni,” amesema.
“Ubadhirifu wa fedha za NHIF Sh3 bilioni na Ubadhilifu wa fedha za NBC Sh4.7 bilioni.
Amesema majalada mengine yaliyokamilika ni pamoja na 100 yaliyotokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), majalada nane yaliyohusu ubadhirifu wa fedha za mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya (uviko 19).