Kitaifa

Kitimoto chapigwa marufuku Ludewa

Ludewa. Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imepiga marufuku uingizwaji wa Nguruwe na matumizi ya mazao yatokanayo na nguruwe wilayani humo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Machi 15, 2023 Daktari wa mifugo wilayani humo Festo Mkomba amesema zuio hilo limekuja baada ya  kubainika kwa uwepo wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe.

Ameongeza  kuwa zuio litadumu mpaka pale itakapotolewa ruhusa kwa wananchi kuanza upya matumizi ya mnyama huyo.

“ Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya mifugo namba 16(2),17 ya mwaka 2003 kuanzia leo 15/03/2023 mimi Dkt. Festo Mkomba (BVM) Daktari wa mifugo Wilaya ya Ludewa natangaza kwamba Ludewa itakuwa chini ya karantini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo, hii ni kutokana na matukio ya ugonjwa wa homa ya nguruwe kujitokeza katika Wilaya ya Ludewa. Amesema Mkomba.

Ameongeza kuwa kwa yeyote atakaye bainika kuendeleza huduma hizi atachukuliwa hatua kali za sheria ambapo moja ya sheria hizo ni kifungo cha miezi sita jela, faini ya sh. Ml. 1,200,000 ama vyote kwa pamoja.

Pia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuutokomeza ugonjwa kwa haraka

“ Naomba tutoe ushirikiano kwenye kuhakikisha hakuna mtu anavunja mashariti yaliyowekwa, kwani tukifanya hivyo huu ugonjwa huwa unaisha haraka sana (unapita) na baada ya hapo tunaendelea na utaratibu wetu wa kuchinja au kula kitimoto kama kawaida.” Amesema Mkomba

Kwa upande wa wananchi wa Ludewa waiomba Halmashauri kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huu ili kupunguza athari zitazo weza letwa.

“ Tunaomba wataalamu wa Halmashauri waje kutoa elimu kwa wananchi ili tuwe na uelewa mpana juu ya huu ugonjwa na hii itasaidia kupunguza hali ya wananchi kujaribu kuingiza au kutumia nyama yake.” Ditmary Mapile.

Kwa upande wake Stephen Magige aiomba Halamsahuri kuchukua hatua kwa wale watakao bainika kuingiza au kutumia nguruwe ili kuepukana na homa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi